HADITHI ZA KWETU
Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Monday, February 11, 2013
RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(3)
Ilikuwa ni siku ya jumanne ,asubuhi na mapema,katika jiji la mwanza ambalo limezungukwa na milima ya aina mbalimbali kama mawe,alimasi na dhahabu.Wingu la kiza na kibari kwa mbali vilitatawla asubuhi ya jumanne.Ilikuwa saa 2 asubuhi,Hamisi alipowasha gari lake na kuelekea mjini.Alipokuwa njiani,gari lake lipata matatizo,baada ya tairi kupasuka katika mpira wa ndani.Hamisi akampigia fundi wa mjini ili waje kumsaidia.Kama tulivyoangalia sehemu iliyopita,tuliona Bakari ndio mpenzi wake Salma.Lakini hatukuweza kufaham Bakari kazi aliokuwa akifanya pale mjini mwanza.Hamisi akampigia fundi anaemuamini kabisa ,ambae ndie Bakari.Kwa wakati huo alikuwa amelala na Salma nyumbani kwake.Simu ilikuwa inaita lakini,Bakari alikuwa usingizini,Salma alikuwa macho pale kitandani,akaishika simu kwa wivu wake kuangalia nani anampigia mpenzi wake mpendwa.Salma akapata mshituko baada ya kuona namba ya Hamisi.Mara Bakari akashtuka usingizini na kumwambia Salma,nipatie simu.Salama akampatia simu Bakari,wakati simu ilikuwa inaita.Bakari akapokea simu na kuongea na Hamisi.Baada ya maongezi Bakari akamgeukia Salma na kumwambia,kuna kazi ya dharura inabidi niende kuifanya haraka,kama utapenda twende wote.
Salma alikwisha fahamu mambo yanavyokwenda na aliyepiga alikwishamtambua ni Hamisi.
Mpaka hapo utaona jinsi gani mapenzi,yalivyokuwa na mzunguko kati ya Bakari na Salma,pamoja na Hamisi na Salma.vilevile utaona kwa upande mwengine,utaona Mwanaidi amekuwa na mpenzi wake Hamisi kwa zaidi ya miaka kumi.Hapo utaona ni hatari sana kwenye mapenzi.na Huyu mfanyabiashara Hamisi ndio anae hudumia mzunguko wote.
RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(SEHEMU YA 2)
Hamisi akalipa pesa za nguo na vipodozi,waondoka kuelekea mjini,Walipofika mjini,wakaingia kwenye hoteli na kuagiza chakula.Baada ya kula chakula ,Hamisi akamchukuwa Salma na kumrudisha nyumbani kwao.Alipofika Salama akaagana na Hamisi.Baada ya hapo salma akaingia ndani kwao.Mama yake salma ,alikuwa akiitwa chausiku,akamkuta ukumbini,na kuanza kusalimiana na mama yake.Salma akaenda moja kwa moja chumbani kwake .
Hamisi alitokea kumenda sana Salma,ndio maana alifanya jitihada zote,ili aweze kuwa na Salma.Kwa upande wa Salma kulikuwa ni tofauti
sana.Salma alikuwa na mpenzi wake Bakari,alikuwa anampenda sana Bakari.Salma akaoga haraka na kuelekea kwa mpenzi wake Bakari.
Baada ya kujiandaa na kuvaa mavazi ya gharama ambayo ,alinunuliwa na mpenzi wake Hamisi.Salma alikuwa amependeza sana.Akaagana na mama yake na kuondoka kuelekea kwa mpenzi wake wa moyoni.
Bakari alikuwa chumbani kwake amejipunzisha,kutokana na uchovu wa kazi za kutwa nzima.
Salma alipofika nyumba anakoishi Bakari akaenda moja kwa moja na kugonga mlango wa Bakari.
Bakari akamkaribisha na wakaenda kitandani kujipunzisha.Salma alikuwa anampenda sana Bakari kupita Bakari anavyompenda Salma.
Kwa wakati huo Hamisi alikuwa yupo nyumbani kwake amejipunzisha na mpenzi wake Mwanaidi.Hamisi na Mwanaidi wamekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka kumi.Kuna mengi mafunzo utayapata katika hadithi hii,kuhusiana na vituko na mambo yanayojitokeza kwa wapenzi duniani kote.
Sunday, February 10, 2013
RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(SEHEMU YA 1)
Katika maisha ya upendo,Salma anakutana na kijana mmoja aitwae Hamisi.Ilikuwa ni siku ya jumatatu asubuhi na mapema,wakati jua lilikuwa linachomoza,ndani ya jiji la Mwanza.Watu walikuwa katika pirika pirika za kuelekea kwenye kutafuta riziki.Katika hali isiyo ya kawaida,Hamisi akiwa ni mfanya biashara mkubwa pale mjini Mwanza,anasimamisha gari yake pembeni mwa Barabara,baada ya kumuona msichana mrembo,akiwa anatembea kwa miguu.
Hamisi akamsalimia yule msichana,dada habari yako?Yule msichana akamjibu nzuri kaka.Hamisi akamuliza yule msichana,dada naona unatembea kwa miguu,sijui unaitwa nani?msichana akamjibu,naitwa Salma,na wewe unaitwa nani?Yule kaka akamjibu,mimi naitwa Hamisi,unaelekea wapi?Salma akamjibu Hamisi,naelekea mjini.Hamisi akamwambia Salma,hata mimi naelekea mjini.panda twende.Salma akaingia kwenye gari,Hamisi akawaswha gari moto na wakaelekea mjini.
Wakiwa njiani,waliweza kuongea maongezi marefu sana,kiasi kwamba walijikuta kana kwamba wanafahamiana kwa muda mrefu sana.Hamisi alitokea kumpenda sana Salma,kutokana na maumbile yake na uzuri wa Salma jinsi ,alivyoumbika.
Kwa upande wa salma alionyesha upendo wa wa kumpenda Hamisi,lakini moyoni hapakuwa na upendo zaidi ya kuwa na tamaa na utajiri alionao Hamisi.
Hamisi akaegesha gari lake pembeni mwa duka la nguo za kike na manukato.Wakashuka wote kwa pamoja na kuingia kwenye duka la nguo na manukato.
Hamisi akamgeukia Salma,napenda ujisikie huru,chagua nguo uipendayo na manukato.pesa ya kulipa ipo usijali.(Sehemu ya pili itaendelea kesho)
http://www.scarlet-clicks.info/banners/banner1.png
Sunday, September 2, 2012
TULIPENDANA KAMA PETE NA KIDOLE(2)
Katika sehemu iliyopita,tumeona Baba sikujua na Mzee chaurembo,wakiwa kwenye kijiwe chao,sehemu ambayo wanakutana mara kwa mara,kwa ajili ya kunywa kahawa pamoja na Jungu kuu,Mzee ambae amekuwa kivutio kikubwa kwa jamii,kwa sababu ya upendo wa dhati aliokuwa nao,kwa mke wake.Baada ya Jungu
kuu kupata kahawa na kuelekea kivukoni,huko ndiko anakofanya kazi,muda mrefu haukupita,mama Rajabu,alipita pale kwenye sehemu wanapokutana kunywa kahawa,na kusalimiana na Mzee chaurembo na Baba sikujua.Baada ya Mama Rajabu kuondoka kuelekea sokoni Buguruni,Mzee chaurembo akamgeukia Baba sikujua,na kumfahamisha kuhusu mama Rajabu,ya kwamba ndio mke wa Jungu kuu.(sasa endelea....)
Christopher ni kijana aliyesoma hadi chuo kikuu,na kuchukua shahada ya uchumi,alikuwa anaishi maeneo ya Mbagala.siku moja wakati akiwa anapita kwenye kijiwe cha kahawa pake Buguruni,akasimama na kusalimiana na wazee pale,kisha Mzee chaurembo akamkaribisha kahawa na kukaa kwenye kiti,kwa ajili ya kunywa kahawa.Wazee walikuwa bado wanataniana kwa maongezi ya hapa na pale.Christopher alipendezewa sana ,na maongezi pale,kisha akauliza samahani wazee,naomba kuuliza kuhusu huyo Jungu kuu,anakaa wapi?
Mzee chaurembo akadakia na kumjibu yule kijana,huyo Jungu kuu anakaa hapa hapa karibu na mgahawa,ila kwa muda huu yupo kazini.ukitaka kuonana nae,njoo asubuhi au jumapili wakati wowote utamwona.
Christopher akapata shauku ya kuja kumwona jumapili.baada ya hapo,akaaga na kuondoka kuelekea Mbagala,alipokuwa anaishi.Ilikuwa majira ya saa 2,usiku Jungu kuu alikuwa bado hajarudi nyumbani.Kawaida hurudi mapema na kupitia kwenye mgahawa,kisha huelekea nyumbani kwake.
Mama Rajabu akaanza kupata wasiwasi,akamtuma mwanae Rajabu,aende pale kwenye mgahawa kwa ,ajili ya kumuangalia Baba yake.Kwa bahati nzuri,Rajabu alipofika kwenye kijiwe cha Kahawa,kabla hajauliza Jungu kuu,akafika pale kijiweni.Jungu kuu akasalimiana na wazee wenzake,kisha akamgeukia mwanae Rajabu,vipi mwanangu mbona uko hapa?Rajabu akamjibu,Mama alinituma nije kukuangalia,kwa sababu alikuwa na wasiwasi na muda mwingi.Baada ya hapo,akaondoka na mwanae kuelekea nyumbani kwake.
Mama Rajabu,akashusha pumzi na kumshukuru mungu.Wakasalimiana na baada ya hapo,akampelekea maji bafuni,kwa ajili mumewe kuoga.Baada ya hapo,wakapata chakula cha usiku,na kuenda kupunzika.Mzee chaurembo na baba sikujua,pamoja na wazee wengine,wakaagana,kila mmoja akaelekea nyumbani kwake.
Friday, August 31, 2012
TULIPENDANA KAMA PETE NA KIDOLE (1)
Ilikuwa kama kawaida yangu,nikitoka nyumbani kuelekea kazini,huwa napita kwenye baraza la kunywa kahawa,katika maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani,kisha baada ya hapo naelekea kivukoni.Siku moja nilitoka nyumbani mapema sana,nikafika maeneo ya kunywa kahawa,majira ya saa moja Asubuhi.Watu wanaokunywa kahawa pale Mnyamani,walikuwa wakinifaham ,kwa jina la utani,kama JUNGU KUU"
Muda huo,mzee chaurembo na Baba sikujua,walikuwa wamekwishafika kwenye kibaraza cha kahawa.Niliwasalimia na kuanza kunywa nao,kahawa.Mzee chaurembo,akamuliza Jungu kuu,hawajambo nyumbani?Jungu kuu akamjibu,Mke wangu hajambo.Baba sikujua akashtuka kidogo,na kumuliza Jungu kuu,mwenzio mzee chaurembo,amekuuliza nyumbani hawajambo?Lakini nashangaa ulivyomjibu kwamba,mke wako hajambo.Kabla jungu kuu ,hajamjibu Baba sikujua,Mzee chaurembo akadakia,unajuwa wewe Baba sikujua,ni kama jina lako,kama ungejua?usingeshangaa na kumuliza Jungu kuu.Mimi huyu ni jirani yangu,Jungu kuu namsifu sana,kwa sababu anajua kumpenda mkewe na si hivyo tu,hata mke wake Jungu kuu,anampenda sana mumewe.Kwa ujumla wanapendana sana.
Muda ulipofika wa kuelekea kazini,Jungu kuu akaondoka na kuelekea kazini.Wakati Jungu kuu,amekwisha ondoka,Baba sikujua akameukia Mzee chaurembo,kumbe mwenzetu anajuwa kupenda kiasi hicho?Mzee chaurembo akamjibu,Barabara Jungu kuu,anajuwa kupenda sio utani.Wakati wakiwa wanaendelea kuongea,Mama Rajabu,ambae ndie ,mke wa Jungu kuu,akapita pale,walipokuwa wanakunywa kahawa.Mama Rajabu,akasimama na kusalimia,kisha Mzee chaurembo,akamuliza Mama Rajabu,unaelekea wapi?Mama Rajabu akamjibu,naelekea sokoni,kununua chakula.Mzee chaurembo,akamwambia mumeo,tulikuwa nae ,muda si mrefu ameelekea kazini.Mzee chaurembo akamwambia Baba sikujua,yule mama alitusalimia sasa hivi,ndio Mke wa,Jungu kuu.
Friday, June 15, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA 12)
Katika sehemu iliyopita tumeona Athumani akijinunulia magazeti,na kukutana na jalada la warembeo,hatimae kufanikiwa kumwona Rehna,ambae ndie mpenzi wake .Kama kawaida yake Athumani,aliweza kumpigia simu Rehna ,na kupanga waonane Bamaga mchana,lakini mkewe Athumani,ambae ni jini,alikuwa akiwasikiliza maongezi yao kwa makini,baada ya hapo Asha alienda kwa njia ya upepo,mpaka chumbani kwa Rehna,alipofika akamkaba Rehna mpaka akaanza kutapika,Asha alifanya hivyo,Lakini Rehna hakuwa akimwona Asha. (sasa endelea.....)
Athumani akaendesha gari mpaka kwenye ufukwe wa bahari,akaiona hoteli nzuri maeneo ya Coco beach.Akaongea na mhudumu wa hoteli,na kuchukuwa chumba namba 23,Wakiwa chumbani wamejipunzisha kitandani,Athumani na Rehna,wakiwa wanashikana sehemu za mwili,Asha akaingia chumbani na kuvua nguo zake,akajitupa kitandani.Athumani akaushika uume wake kuingiza kwa Rehna,Lakini Asha akaudhika na kuingiza yeye mahala pake,kisha Asha akachukuwa mkono wake na kuuingiza sehemu ya Rehna,Ilikuwa ni mbinu ya khali ya juu,aliyotumia jini Asha.Kwa mkono wa Asha aliweza kuukunja na kuupekecha mpaka Rehna akawa anasikia maumivu makali badala ya starehe.Rehna akamwambia Athumani ,mbona unaniumiza?
Athumani akamjibu Rehna vumilia baby,mbona mimi najisikia raha kama nikiwa na mke wangu.(nini kitatokea?angalia sehemu ijayo)
Tuesday, June 12, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA KUMI NA MOJA)
Katika sehemu ya kumi tumeona jinsi alivyopata msukosuko wa moyo,baada ya kushuhudia tukio,ambalo ,bado anajiuliza mpaka leo,hivi yule nilyemuona amekumbatiwa na jamaa,alikuwa mke wangu?jibu hajalipata,ila endelea sehemu hii,utapata ukweli wa mambo.(sasa endelea.....)
Mwandishi wa kujitegemea Thomas,alifanikiwa kutoa jalada maalumu,katika gazeti la warembo,kwa ajili ya kumzungumzia Rehna.Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi,gazeti la warembo lilikwisha sambaa mitaani.Athumani kwa muda huo,alikuwa akielekea kazini,akiwa njiani,aliweza kujinunulia magazeti 2,uhuru na mzalendo,katika kupitisha macho kwenye meza ya magazeti,akaona picha kubwa ya binti,anakuja kwenye hisia,kama kuna sehemu,alikwisha muona.Akachukuwa nakala moja,akaangalia kwa makini na kusoma,akaona maelezo yako sahii,ni kweli anamfaham binti yule,Rehna.Akajinunulia nakala moja inayomzungumzia Rehna,na kupanda gari,kulekea kazini.Athumani alipofika kazini,akachukuwa simu yake ,na kumpigia Rehna.Wakasalimiana na kukumbushana siku waliyokuwa pamoja coco beach.
Athumani akampongeza Rehna,hongera nimeona umetoka kwenye gazeti la warembo.Rehna akamjibu Athumani,sina taarifa yeyote juu ya jalada la warembo.Athumani akamwambia Rehna,usijali ninalo,nitakupa baadae.naomba tuonane Bamaga majira ya mchana.Rehna akamjibu sawa dear.
Asha mke wa Athumani alikuwa ni jini,ambae hakutaka mumewe Athumani ajuwe kwamba yeye ni jini.watu wengi wamekuwa wakiishi na majini,pasipo kuelewa.hii imesababisha mifarakano mingi katika ndoa.Wakati Athumani akiongea na Rehna,Asha ambae ndie mke wa Athumani,alikuwa palepale ofisini,akimsikiliza mumewe.Asha akatafakari nini afanye,akaondoka mpaka nyumbani kwa Rehna.Alipofika akaingia kama upepo,mpaka chumbani kwa Rehna,Asha akamkaba Rehna shingoni,mpaka Rehna akajisikia uchungu kama anakufa,akamuachia.Rehna akaanza kutapika,mfululizo,Asha alikuwa amesimam anacheka,kumbuka Asha ndie anamuona Rehnna.(nini kitatokea?endelea sehemu ifuatayo
Subscribe to:
Posts (Atom)