Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Monday, June 11, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI( SEHEMU YA TISA)
Katika sehemu iliyopita tumeona Polisi baada,ya kupewa taarifa za wizi,waliweza kufanikiwa kuwakamata wahalifu wote,waliohusika kwenye uvamizi wa nyumba ya Athumani.Waliweza kufikishwa kituoni,kwa ajili ya kufungua jalada la kesi,ili kuipeleka kesi mahakamani.(sasa endelea......)
Ilikuwa ni siku ya jumanne asubuhi,Thomas ambae alikuwa ni mwandishi wa habari wa kujitegemea,alikuwa katika pita zake mitaani,akakutana na msichana mrembo,aliyejulikana kwa jina la Rehna.Wakati Thomas alipokutana na Rehna,ilikuwa nje kidogo ya nyumbani kwao.Thomas akamsalimia Rehna,hujambo dada?Rehna akamjibu sijamba Kaka.Thomas akajitambulisha kwa Rehna kama ifutavyo,Samahani dada,Naitwa Thomas,ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.Rehna akamjibu,nashkuru kwa kunifahamisha,naitwa Rehna,ni mwanafunzi.
Thomas akamwambia Rehna,napenda nipate maelezo yako kwa ujumla,pamoja na picha nitakupiga,wewe ndio mrembo utakaonekana kwenye gazeti la warembo.Rehna akatoa maelezo yote na kumpatia Thomas.baada ya maelezo,Thomas akampiga picha 4.Alipomaliza akachukuwa namba ya simu,wakaagana.
Athumani aliondoka,nyumbani kwake kwa ajili ya kuelekea kazini.Alipofika kazini akaendela na kazi mpaka majira ya saa 7 mchana.Baada ya hapo,akaelekea kituoni,kwa ajili ya kujuwa siku ya kesi.Alipofika kituoni,akakutana na Afisa mpelelezi na kupewa maelezo kamili.Athumani alitakiwa kuhudhuria kesi mahakamani tarehe 12 julai.
Athumani akaondoka kuelekea nyumbani.Alipofika nyumbani kwake,akamkuta mke wake,hayupo.
Athumani akampigia simu mkewe,lakini simu ya mkewe ilikuwa haipatikani.Athumani akatoka nyumbani na kuendesha gari mpaka mjini.Alikuwa akiendesha gari,huku akitupa macho yake pande zote mbili.Ghafla akamuona mkewe amekaa kwenye kiti pembeni mwa hoteli,akiwa amekumbatiana na Jamaa mmoja mnene.(nini kitatokea?angalia sehemu ya kumi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment