Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Tuesday, June 12, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA KUMI NA MOJA)
Katika sehemu ya kumi tumeona jinsi alivyopata msukosuko wa moyo,baada ya kushuhudia tukio,ambalo ,bado anajiuliza mpaka leo,hivi yule nilyemuona amekumbatiwa na jamaa,alikuwa mke wangu?jibu hajalipata,ila endelea sehemu hii,utapata ukweli wa mambo.(sasa endelea.....)
Mwandishi wa kujitegemea Thomas,alifanikiwa kutoa jalada maalumu,katika gazeti la warembo,kwa ajili ya kumzungumzia Rehna.Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi,gazeti la warembo lilikwisha sambaa mitaani.Athumani kwa muda huo,alikuwa akielekea kazini,akiwa njiani,aliweza kujinunulia magazeti 2,uhuru na mzalendo,katika kupitisha macho kwenye meza ya magazeti,akaona picha kubwa ya binti,anakuja kwenye hisia,kama kuna sehemu,alikwisha muona.Akachukuwa nakala moja,akaangalia kwa makini na kusoma,akaona maelezo yako sahii,ni kweli anamfaham binti yule,Rehna.Akajinunulia nakala moja inayomzungumzia Rehna,na kupanda gari,kulekea kazini.Athumani alipofika kazini,akachukuwa simu yake ,na kumpigia Rehna.Wakasalimiana na kukumbushana siku waliyokuwa pamoja coco beach.
Athumani akampongeza Rehna,hongera nimeona umetoka kwenye gazeti la warembo.Rehna akamjibu Athumani,sina taarifa yeyote juu ya jalada la warembo.Athumani akamwambia Rehna,usijali ninalo,nitakupa baadae.naomba tuonane Bamaga majira ya mchana.Rehna akamjibu sawa dear.
Asha mke wa Athumani alikuwa ni jini,ambae hakutaka mumewe Athumani ajuwe kwamba yeye ni jini.watu wengi wamekuwa wakiishi na majini,pasipo kuelewa.hii imesababisha mifarakano mingi katika ndoa.Wakati Athumani akiongea na Rehna,Asha ambae ndie mke wa Athumani,alikuwa palepale ofisini,akimsikiliza mumewe.Asha akatafakari nini afanye,akaondoka mpaka nyumbani kwa Rehna.Alipofika akaingia kama upepo,mpaka chumbani kwa Rehna,Asha akamkaba Rehna shingoni,mpaka Rehna akajisikia uchungu kama anakufa,akamuachia.Rehna akaanza kutapika,mfululizo,Asha alikuwa amesimam anacheka,kumbuka Asha ndie anamuona Rehnna.(nini kitatokea?endelea sehemu ifuatayo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment