Translate

Friday, June 8, 2012

NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA TATU)

Katika sehemu iliyopita tumeona Athumani na rafiki yake Thomas.Alikuwa Thomas ndio aliyemkaribisha Athumani nyumbani kwake,kwa ajili ya chakula cha mchana.Baada ya Thomas ,kumtambulisha Athumani kwa mke wake na binti zake wawili,Athumani alivitiwa sana na binti wake rehna ,kwa sababu alikuwa na mvuto wa kupendeza.(sasa endelea......) Athumani akaingiza gari ndani,na kufunga mlango mkubwa.Kama kawaida yake Asha akamkumbatia mumewe na kumpa busu la nguvu.Baada ya hapo ,Asha akaenda bafuni na kumpelekea maji,kwa ajili ya mumewe kuoga.Alipomaliza kuweka maji bafuni,akaenda chumbani,na kumwambia Mumewe ,aende bafuni kuoga.Athumani akachukuwa taulo,na kuelekea bafuni kuoga.Wakati huo ,Asha alichukuwa chakula na kupeleka sebuleni,kwa ajii ya mumewe kupata chakula cha jioni.Athumani alipomaliza kuoga na akaenda sebuleni ,kupata chakula na mkewe.Baada ya chakula wakaenda chumbani kujipunzisha.Thomas alikuwa nyumbani kwake na familia yake.Athumani alijitupa kitandani na mke wake Asha.Baada ya muda Asha akawa amelala hoi.Athumani akatuma ujumbe mfupi kwa Rehna.hujambo mtoto mzuri?Rehna alipopata ujumbe kutoka kwa Athumani ,akamjibu ,na kumwambia,sijambo dear wangu.Athumani baada ya kuona majibu ya haraka kwa Rehna,Athumani akatuma ujumbe mwengine kwa Rehna,sikiliza baby,nimetokea kukupenda sana ,wewe ni mrembo,mzuri wa kuvutia,naomba unikubalie penzi langu kwako,nami nitakuwa mwenye furaha,na upendo wa dhati kwako.kisha akautuma ujumbe huo kwa Rehna.Ujumbe ulipomfikia Rehna,akausoma kwa makini sana.kisha akaujibu kama ifuatavyo,sikiliza dear wangu,hata mimi nimekupenda sana,ila naomba uwe kweli na usinidanganye ,nitakupa penzi la kweli.(nini

No comments: