Translate

Friday, June 8, 2012

NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA NNE)

Katika sehemu iliyopita tumeona Athumani akiagana na Thomas,baada ya chakula,kisha Athumani kurejea nyumbani kwake na kukutana na mke wake Asha,Baada ya kusalimina Asha akaenda bafuni kumpelekea maji ya kuoga.Wakati mumewe akiwa anaoga,Asha alikwenda kuweka chakula sebuleni.Athumani alipomaliza kuoga,akaenda sebuleni kula chakula na mke wake.Walipomaliza kula chakula,wakaenda chumbani kujipunzisha.Baada ya muda ,Asha alikuwa amelala usingizi.(sasa endelea.....) Baada ya Athumani kupata ujumbe kutoka kwa Rehna,alifurahi sana,kuona kwamba upo uwezekano mkubwa wa kumpata Rehna.Akavuta pumzi na kunza kuandika ujumbe kwa Rehna.Sikiliza Rehna,mimi nimekupenda kutoka moyoni,naomba kesho jumapili tuonane.kisha akautuma kwa Rehna.Baada ya kupokea ujumbe huo,Rehna akaujibu,kama ifuatavyo,baby usiwe na wasiwasi,nifuate Bamaga ,saa nne asubuhi.kisha akautuma kwa Athumani.Baada ya kupata ujumbe huo,Athumani akamjibu Rehna kama ifuatavyo,usiwe na khofu,nitafika muda huo.kisha akamwambia nakutakia usiku mwema.tutaonana kesho.kisha akamtuia Rehna.Ujumbe ulimfikia Rehna akiwa na usingizi mwingi,baada ya kusoma ujumbe,akamjibu .Ahsante dear wangu usiku mwema.Rehna akalala usingizi,Asubuhi na mapema,Asha akaamka na kutayarisha maji ya kuoga.Athumani a kaenda bafuni kuoga,Wakati huo ,Asha alikuwa anatayarisha chai ya asubuhi.Baada ya kumaliza kuoga na kuvaa nguo,Athumani akaenda sebuleni kunywa chai.Baada ya kunywa chai,ilikuwa majira ya saa tatu na nusu,Athumani akamuaga mke wake,naenda mjini mara moja,kuna mtu naenda kufanya nae mazungumzo.Asha akamjibu mumewe,sawa ila usichelewe mume wangu.Athumani akamjibu,sitochele9wa mke wangu.Athumani akawasha gari moto,na kuelekea Bamaga.(nini kitatokea?endelea sehemu ya tano)

No comments: