Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Friday, June 8, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA TANO)
NAMPENDA KUTOKA MOYONI :SEHEMU YA TANO
Katika sehemu iliyopita tumeona Athumani,akiwa anatumiana ujumbe mfupi na Rehna ,na kukubaliana kukutana Bamaga siku ya pili.(sasa endelea...)
Athumani alikuwa anaendesha gari lake taratibu,akiwa anaelekea Bamaga.Rehna aliondoka nyumbani kwao mapema,baada ya kuaga anaenda kanisani.Athumani alifika Bamaga na kumkuta Rehna akiwa amekwishafika anamsubiri.baada ya kukutana uso kwa uso,wakapeana mikono na kukumbatiana.Athumani akamwambia Rehna ,ingia kwenye gari,tukatembee Baharini.Rehna akaingia kwenye gari,na wakaelekea Baharini.walienda mpaka COCO BEACH.Athumani akaegesha gari lake pembeni,na wakaanza kutembea ufukweni mwa bahari,wakiwa wameshikana mikono.Waliendelea na starehe zao ,mpaka majira ya saa saba mchana.ndipo walipoamua kuondoka baharini.Athumani akawasha gari moto,na kumpeleka Rehna mpaka karibu na nyumbani kwao.Athumani alipomfikisha Rehna kwao,akaondoka kuelekea nyumbani kwake.Asha alikuwa anatayarisha chakula cha mchana,mara akasikia sauti ya gari la mumewe,akaenda kufungua mlango wa geti,Athumani akaingiza gari mpaka ndani.Asha akamwambia mumewe,nilikuwa nikupigie simu,lakini kabla sijafanya hivyo ukatokea.Athumani akamjibu mkewe,samahani kwa kuchelewa,mazungumzo yalikuwa marefu kidogo.Asha akaweka chakula sebuleni,wote kwa pamoja wakaanza kula chakula cha mchana.Kwa upande mwengine Rehna alikuwa amechanganyikiwa sana na Athumani.alikuwa na anatamani kuwa na Athumani muda mrefu zaidi.(nini kitatokea?sasa endelea sehemu ya sita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment