Translate

Saturday, June 9, 2012

NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA SITA)

Katika sehemu iliyopita tumeona Rehna na Athumani wakiwa Coco beach,kwa ajili ya kujipunzisha kwa muda,kisha baadae ,majira ya saa 7 ,mchana waliondoka kuelekea nyumbani,Athumani alimfikisha Rehna nyumbani kwao,kisha akaelekea nyumbani kwake,alipofika nyumbani,mke wake Asha,akafungua geti la nyumba,kisha Athumani akaingiza gari ndani,Baada ya hapo,wakakaa sebuleni na kula chakula pamoja.(sasa endelea.....) Ilikuwa ni siku ya jumatatu asubuhi,majira ya saa 2,kikundi cha watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa Athumani,na kupora vitu vingi vya thamani,lakini hakuna madhara ya kumjerui mtu yeyote hapo nyumbani kwake,Athumani na mkewe Asha,waliomba usalama wa roho zao,bila kujali hasara ya vitu watakavyochukuwa.Baada ya dakika 20,kundi hilo likatoweka na mali na kukimbilia mji mwengine,kwa mwendo wa haraka.Athumani alimwambia mkewe,usihudhunike,pesa ni makaratasi,hasara ni roho.Asha alikuwa na mawazo mengi ya tukio kama hilo,lakini hakuweza kupata majibu ya haraka.Alifikiria mambo mengi sana,na kujaribu kufikiri,nini chanzo cha tukio,lakini mawazo yote,hayakuweza kumpa majibu.Athumani akamwambia mkewe ajitayarishe,wapate kutoka pamoja,kwa sababu,haitakuwa jambo jema kubaki peke yake,kwa tukio ambalo limetokea.Asha akaingia chumbani kutafuta nguo,atakayoweza kuipata,ili aweze kuvaa. Baada ya muda kidogo,wakaondoka hapo nyumbani,kuelekea mjini.

No comments: