Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Friday, June 8, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA KWANZA)
Katika maisha yangu ,tokea nikiwa mdogo,wakati nikiwa kijijini kwetu mwera,nilitokea kuwa rafiki mkubwa wa Athumani,wakati huo ,nilikuwa na miaka 7,na Athumani alikuwa na miaka 12,Katika familia yetu ya mzee jabiri,tumezaliwa 2,mimi asha,na aziza wa mwisho.Athumani na mimi ,tulibahatika kusoma shule moja ya msingi mwera,lakini ,Athumani alimaliza kwanza na kuendelea na sekondari ya Galanose iliyoko mjini Tanga.Miaka 4 ,baadae nami nikamaliza shule ya msingi na kuchaguliwa kwenda shule ya wasichana korogwe.Mahusiano yetu ,yalikuwa yakiendelea,kadri siku zilivyokuwa zikienda mbele.baada ya kuhitimu chuo kikuu,Athumani alipata kazi wizara ya viwanda na biashara,na alikuwa akifanya kazi Dare-sSalaam.Nilifanikiwa kumaliza kidato cha sita ,na sikubahatika kwenda chuo.Ndipo Athumani alipoamua kufunga ndoa na mimi.Miaka miwili baadae,tukafunga ndoa na kuanza maisha mapya ya ndoa mjini Dare-sSalaam.Kama mnavyoelewa maisha ya mjini yana misukosuko mingi na mambo mengi.Athumani alikuwa akifanya kazi kama afisa masoko wizarani,kazi ambayo ilikuwa na maslahi makubwa zaidi.Aliweza kubadilika kimaisha na kujenga nyumba nzuri maeneo ya Gongo la mboto,na pia alikuwa na usafiri wake mwenyewe.Kwa ujumla maisha ya Asha na Athuman,kama mke na mume,yalikuwa mazuri sana.Majirani zao,pia walikuwa wanajuwa upendo waliokuwa nao Asha na Athuman.(nini kitatokea?endelea sehemu ya pili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment