Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Friday, June 8, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA PILI)
Katika sehemu ya kwanza tumeona Asha na Athumani wakiwa shuleni,hadi kufika wakati wakawa na uamuzi wa kuishi kama mke na mume,baada ya kufunga ndoa,na kuanza maisha yao DaresSalaam.Athumani alikuwa Afisa masoko wizarani.Maisha yao ,yalikuwa mazuri sana.(sasa endelea.....)
Thomas ni katibu mkuu ,wizara ya viwanda na biashara,alikuwa ni rafiki mkubwa wa Athumani,Thomas alikuwa ni mtu mwenye msaada mkubwa kwa Athumani,na ndiye aliyefanya mipango ya kazi kwa Athumani.Siku moja Thomas ,alimualika nyumbani kwake Athumani,kwa ajili ya chakula cha mchana.Athumani alifika kwa Thomas muda muwafaka,Thomas akaanza kumtambulisha Athumani kwa mke wake Irene,baada ya hapo ,akawaita watoto wake wawili,ambao wote ni mabinti,Maria na Rehna.Athumani alipowaangalia wale mabinti,alivutiwa sana na Rehna kwa uzuri,aliokuwa nao.Rehna alikuwa na miaka 19,mwenye umbo la kuchanganya mwanaume yeyote duniani.Thomas akamkaribisha chakula Athumani,na wakaanza kula chakula.Baada ya chakula,thomas alikwenda chumbani kuongea na mke wake,muda huo Rehna alikuwa yupo na Athumani,Bila kuchelewa Athumani akamwambia Rehna chukuwa namba yangu ya simu,nitakuwa na maongezi na wewe.Rehna akachukuwa namba ya simu ,na akampatia namba yake.Thomas akatoka nje,na wakaagana na Athumani.Baada ya kuagana Athumani,akawasha gari moto na kuelekea nyumbani kwake.Alipofika akamkuta mkewe Asha ,ndio anamalizia kupika chakula.(nini kitatokea?sasa endelea sehemu ya tatu)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment