Translate

Saturday, June 9, 2012

NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA SABA)

Katika sehemu iliyopita tumeona nyumbani kwa Athumani,kundi la watu wasiojulikana,lilivamia na kupora vitu mbalimbali,lakini hapakuwa na majeruhi yeyote karika tukio hilo.Baada ya tukio,Athumani na mkewe Asha wakaondoka kuelekea mjini.(sasa endelea.....) Athumani aliendesha gari taratibu mpaka mjini,akaenda kwa tajiri yake kutoa taarifa,baada ya hapo,Athumani na mkewe Asha,wakaelekea kituo cha polisi,kwa ajili ya kutoa taarifa, kamili ya tukio lililotokea nyumbani kwao.kisha baada ya hapo wakaelekea ufukweni mwa bahari kwa ajili ya kupunguza mawazo.Athumani alikuwa akifikiria jumapili alipokuwa na Rehna,wakati Asha alikuwa mwenye furaha,kwa sababu,ni kipindi kirefu,alikuwa hajawahi kufika maeneo ya ufukwe wa bahari. Majira ya saa 9,mchana ,Athumani akamuliza mke wake,unafikiri ni sababu gani,tumepata tukio kama hili?Asha akamjibu mumewe,kwa kweli mpaka muda huu,nimekuwa nafikiri,na kuwaza lakini jibu bado sijalipata.Athumani akamuliza tena Asha,unae rafiki wa karibu,anaekuja nyumbani kukutembelea?Asha akamjibu mumewe,ninae rafiki mmoja,lakini anakaa mbali kidogo. Athumani akamwambia Asha,tuondoke mara moja.Wakapanda kwenye gari na kuondoka.Athumani akaenda mpaka kituo cha polisi,wakatoa taarifa ya huyo msichana.polisi 4,wakaondoka nao,na kuelekea nyumbani kwa msichana huyo,aliyejulikana kwa jina la chiku.Walipofika nyumbani kwa chiku,polisi wakaizunguka nyumba yote,wakatoa tangazo maalumu.(nini kitatokea?endelea sehemu ya nane)

No comments: