Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Sunday, June 10, 2012
NAMPENDA KUTOKA MOYONI(SEHEMU YA NANE)
Katika sehemu iliyopita tumeona tukio lililotokea nyumbani kwa Athumani,baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia hapo nyumbani kwa Athumani,na kupora vitu mbalimbali,baada ya tukio,Athumani na mkewe Asha,wakaondoka kuelekea mjini,na kuripoti kituo cha polisi,kisha sehemu anayofanyia kazi,baada ya hapo,wakaelekea baharini kwa ajili ya kujipunzisha.Wakiwa huko,Athumani alimuliza mkewe,kama ana upo wowote,kuhusu tukio zima kwa ujumla,kisha wakapata wazo,huwenda rafiki yake Asha,akawa chanzo cha tukio.Wakaondoka kuelekea kituo cha polisi kuripoti,Polisi wakaamua kwenda nao mpaka nyumbani kwa chiku.Walipofika wakaizingira nyumba,na kutoa tangazo maalum.(sasa endelea.....)
Polisi waliamuru kila mtu aliye katika nyumba ile,atoke kwa usalama wake,kabla jeshi la polisi ,halijachukuwa mkondo wake wa sheria.Watu wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine,kulikuwa na watu 12,ndani ya nyumba ile,wengine 3,walikuwa wapangaji katika nyumba ile.Kati ya hao,wale wote waliokuja kupora nyumbani kwa Athumani.Baada ya wote kutoka,polisi akamuliza Athumani,je unawafahamu hawa?Athumani akajibu,hawa sita ndio waliokuja kupora asubuhi ya leo,nyumbani kwangu.Polisi wakawatia pingu wale wote sita,pamoja na chiku.Kisha polisi akawauliza wale waporaji,vitu viko wapi?
mmoja wao akajibu,vipo ndani chumbani kwa chiku.
Polisi na Athumani,wakaelekea ndani ya chumba cha chiku,waliweza kukuta vitu vingi,pamoja na silaha za kila aina,ndani ya chumba.Wakatoa vitu vyote na kuvipakia kwenye gari,kisha wakaelekea kituoni.Walipofika kituoni wakfungua kesi zidi ya waporaji,na kuandaa jalada,kwa ajili ya kuipeleka kesi mahakamani.
Athumani akamwambia mkewe Asha,umeona faida ya mashoka kama hawa?Asha akamjibu mumewe,yaani sikutegemea,kweli kikulacho.....ni kinguoni mwako.Kwa hili mume wangu nimejifunza mengi sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment