Translate

Tuesday, June 12, 2012

NAMPENDA KUTOKA MOYONI-(SEHEMU YA KUMI)

Katika sehemu ya tisa.tumeona Thomas,akikutana na Mrembo Rehna,Baada ya ktambulishana,akachukuwa maelezo ya Rehna na picha,kwa ajili ya kwenda kutoa kwenye gazeti la warembo.pia tumeona Athumani akienda kituoni kwa ajili ya kupata taarifa za kesi na siku ya kwenda kuhudhuria mahakamani,baada ya hapo,athumani alirejea nyumbani kwake,lakin hakuweza kumkuta mke wake.akampigia simu,lakini ilikuwa haipatikani,mwisho akaondoka na gari kuelekea mjini.Aliendesha gari taratibu,huku akiangaza huku na kule,akamwona mke wake amekaa pembeni mwa hoteli na jamaa mnene ,akiwa amemkumbatia mkewe.(sasa endelea....) Athumani akasogeza gari mpaka pale karibu na mkewe na jamaa walipokaa.Athumani akashuka kwenye gari akiwa na hasira nyingi,alipokaribia akaona kibibi kizee,kinalia.palepale alipokaa mkewe na jamaa yake,akaangaza macho pande zote nne,hakuweza kumwona mke wake ,wala yule jamaa.Athumani akashangaa sana,yule bibi akamuliza Athumani ,una matatizo gani mjukuu wangu?Athumani akamjibu,kuna jamaa alikuwa na mwanamke wamekaa hapo ulipo kaa,nashangaa nimeshuka kwenye gari siwaoni,nakuona wewe.Bibi akamjibu Athumani,sikiliza mjukuu wangu,hapa mimi nipo tokea jana kwenye kiti hichi,hakuna mtu mwengine aliyekaa hapa.Athumani akafikiria sana,mara simu ikawa inalia,kuangalia namba ,akaiona simu ya mke wake Asha,Hakuweza kuamini akapokea simu,Atumani akamuliza mke wake,uko wapi?Asha akamjibu mimi nipo nyumbani.Athumani akamuiza tena Asha,mbona nilikuja sijakuona?Asha akamjibu,nilikuwa nyumba ya pili,nilienda kusuka.Athumani akawasha gari na kuelekea nyumbani kwake,Alipofika akamkuta mkewe.Athumani alikuwa na hasira lakini ,hakuwa na ushaidi kamili wa tukio la mkewe.Asha akamtayarishia chakula,baada ya hapo,wakawa wanakula chakula pamoja.Athumani alimpenda kutoka moyoni Asha,lakini bado ,hajatambua kwamba Asha ni jini.Mengi ya kusisimua tutayaona baadae.wakati ,Athumani akiwa anajaribu kumsaliti, Asha na wapenzi wengine.

No comments: