Translate

Friday, August 31, 2012

TULIPENDANA KAMA PETE NA KIDOLE (1)

Ilikuwa kama kawaida yangu,nikitoka nyumbani kuelekea kazini,huwa napita kwenye baraza la kunywa kahawa,katika maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani,kisha baada ya hapo naelekea kivukoni.Siku moja nilitoka nyumbani mapema sana,nikafika maeneo ya kunywa kahawa,majira ya saa moja Asubuhi.Watu wanaokunywa kahawa pale Mnyamani,walikuwa wakinifaham ,kwa jina la utani,kama JUNGU KUU" Muda huo,mzee chaurembo na Baba sikujua,walikuwa wamekwishafika kwenye kibaraza cha kahawa.Niliwasalimia na kuanza kunywa nao,kahawa.Mzee chaurembo,akamuliza Jungu kuu,hawajambo nyumbani?Jungu kuu akamjibu,Mke wangu hajambo.Baba sikujua akashtuka kidogo,na kumuliza Jungu kuu,mwenzio mzee chaurembo,amekuuliza nyumbani hawajambo?Lakini nashangaa ulivyomjibu kwamba,mke wako hajambo.Kabla jungu kuu ,hajamjibu Baba sikujua,Mzee chaurembo akadakia,unajuwa wewe Baba sikujua,ni kama jina lako,kama ungejua?usingeshangaa na kumuliza Jungu kuu.Mimi huyu ni jirani yangu,Jungu kuu namsifu sana,kwa sababu anajua kumpenda mkewe na si hivyo tu,hata mke wake Jungu kuu,anampenda sana mumewe.Kwa ujumla wanapendana sana. Muda ulipofika wa kuelekea kazini,Jungu kuu akaondoka na kuelekea kazini.Wakati Jungu kuu,amekwisha ondoka,Baba sikujua akameukia Mzee chaurembo,kumbe mwenzetu anajuwa kupenda kiasi hicho?Mzee chaurembo akamjibu,Barabara Jungu kuu,anajuwa kupenda sio utani.Wakati wakiwa wanaendelea kuongea,Mama Rajabu,ambae ndie ,mke wa Jungu kuu,akapita pale,walipokuwa wanakunywa kahawa.Mama Rajabu,akasimama na kusalimia,kisha Mzee chaurembo,akamuliza Mama Rajabu,unaelekea wapi?Mama Rajabu akamjibu,naelekea sokoni,kununua chakula.Mzee chaurembo,akamwambia mumeo,tulikuwa nae ,muda si mrefu ameelekea kazini.Mzee chaurembo akamwambia Baba sikujua,yule mama alitusalimia sasa hivi,ndio Mke wa,Jungu kuu.