Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Sunday, September 2, 2012
TULIPENDANA KAMA PETE NA KIDOLE(2)
Katika sehemu iliyopita,tumeona Baba sikujua na Mzee chaurembo,wakiwa kwenye kijiwe chao,sehemu ambayo wanakutana mara kwa mara,kwa ajili ya kunywa kahawa pamoja na Jungu kuu,Mzee ambae amekuwa kivutio kikubwa kwa jamii,kwa sababu ya upendo wa dhati aliokuwa nao,kwa mke wake.Baada ya Jungu
kuu kupata kahawa na kuelekea kivukoni,huko ndiko anakofanya kazi,muda mrefu haukupita,mama Rajabu,alipita pale kwenye sehemu wanapokutana kunywa kahawa,na kusalimiana na Mzee chaurembo na Baba sikujua.Baada ya Mama Rajabu kuondoka kuelekea sokoni Buguruni,Mzee chaurembo akamgeukia Baba sikujua,na kumfahamisha kuhusu mama Rajabu,ya kwamba ndio mke wa Jungu kuu.(sasa endelea....)
Christopher ni kijana aliyesoma hadi chuo kikuu,na kuchukua shahada ya uchumi,alikuwa anaishi maeneo ya Mbagala.siku moja wakati akiwa anapita kwenye kijiwe cha kahawa pake Buguruni,akasimama na kusalimiana na wazee pale,kisha Mzee chaurembo akamkaribisha kahawa na kukaa kwenye kiti,kwa ajili ya kunywa kahawa.Wazee walikuwa bado wanataniana kwa maongezi ya hapa na pale.Christopher alipendezewa sana ,na maongezi pale,kisha akauliza samahani wazee,naomba kuuliza kuhusu huyo Jungu kuu,anakaa wapi?
Mzee chaurembo akadakia na kumjibu yule kijana,huyo Jungu kuu anakaa hapa hapa karibu na mgahawa,ila kwa muda huu yupo kazini.ukitaka kuonana nae,njoo asubuhi au jumapili wakati wowote utamwona.
Christopher akapata shauku ya kuja kumwona jumapili.baada ya hapo,akaaga na kuondoka kuelekea Mbagala,alipokuwa anaishi.Ilikuwa majira ya saa 2,usiku Jungu kuu alikuwa bado hajarudi nyumbani.Kawaida hurudi mapema na kupitia kwenye mgahawa,kisha huelekea nyumbani kwake.
Mama Rajabu akaanza kupata wasiwasi,akamtuma mwanae Rajabu,aende pale kwenye mgahawa kwa ,ajili ya kumuangalia Baba yake.Kwa bahati nzuri,Rajabu alipofika kwenye kijiwe cha Kahawa,kabla hajauliza Jungu kuu,akafika pale kijiweni.Jungu kuu akasalimiana na wazee wenzake,kisha akamgeukia mwanae Rajabu,vipi mwanangu mbona uko hapa?Rajabu akamjibu,Mama alinituma nije kukuangalia,kwa sababu alikuwa na wasiwasi na muda mwingi.Baada ya hapo,akaondoka na mwanae kuelekea nyumbani kwake.
Mama Rajabu,akashusha pumzi na kumshukuru mungu.Wakasalimiana na baada ya hapo,akampelekea maji bafuni,kwa ajili mumewe kuoga.Baada ya hapo,wakapata chakula cha usiku,na kuenda kupunzika.Mzee chaurembo na baba sikujua,pamoja na wazee wengine,wakaagana,kila mmoja akaelekea nyumbani kwake.
Subscribe to:
Posts (Atom)