Translate

Monday, February 11, 2013

RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(3)

Ilikuwa ni siku ya jumanne ,asubuhi na mapema,katika jiji la mwanza ambalo limezungukwa na milima ya aina mbalimbali kama mawe,alimasi na dhahabu.Wingu la kiza na kibari kwa mbali vilitatawla asubuhi ya jumanne.Ilikuwa saa 2 asubuhi,Hamisi alipowasha gari lake na kuelekea mjini.Alipokuwa njiani,gari lake lipata matatizo,baada ya tairi kupasuka katika mpira wa ndani.Hamisi akampigia fundi wa mjini ili waje kumsaidia.Kama tulivyoangalia sehemu iliyopita,tuliona Bakari ndio mpenzi wake Salma.Lakini hatukuweza kufaham Bakari kazi aliokuwa akifanya pale mjini mwanza.Hamisi akampigia fundi anaemuamini kabisa ,ambae ndie Bakari.Kwa wakati huo alikuwa amelala na Salma nyumbani kwake.Simu ilikuwa inaita lakini,Bakari alikuwa usingizini,Salma alikuwa macho pale kitandani,akaishika simu kwa wivu wake kuangalia nani anampigia mpenzi wake mpendwa.Salma akapata mshituko baada ya kuona namba ya Hamisi.Mara Bakari akashtuka usingizini na kumwambia Salma,nipatie simu.Salama akampatia simu Bakari,wakati simu ilikuwa inaita.Bakari akapokea simu na kuongea na Hamisi.Baada ya maongezi Bakari akamgeukia Salma na kumwambia,kuna kazi ya dharura inabidi niende kuifanya haraka,kama utapenda twende wote. Salma alikwisha fahamu mambo yanavyokwenda na aliyepiga alikwishamtambua ni Hamisi. Mpaka hapo utaona jinsi gani mapenzi,yalivyokuwa na mzunguko kati ya Bakari na Salma,pamoja na Hamisi na Salma.vilevile utaona kwa upande mwengine,utaona Mwanaidi amekuwa na mpenzi wake Hamisi kwa zaidi ya miaka kumi.Hapo utaona ni hatari sana kwenye mapenzi.na Huyu mfanyabiashara Hamisi ndio anae hudumia mzunguko wote.

RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(SEHEMU YA 2)

Hamisi akalipa pesa za nguo na vipodozi,waondoka kuelekea mjini,Walipofika mjini,wakaingia kwenye hoteli na kuagiza chakula.Baada ya kula chakula ,Hamisi akamchukuwa Salma na kumrudisha nyumbani kwao.Alipofika Salama akaagana na Hamisi.Baada ya hapo salma akaingia ndani kwao.Mama yake salma ,alikuwa akiitwa chausiku,akamkuta ukumbini,na kuanza kusalimiana na mama yake.Salma akaenda moja kwa moja chumbani kwake . Hamisi alitokea kumenda sana Salma,ndio maana alifanya jitihada zote,ili aweze kuwa na Salma.Kwa upande wa Salma kulikuwa ni tofauti sana.Salma alikuwa na mpenzi wake Bakari,alikuwa anampenda sana Bakari.Salma akaoga haraka na kuelekea kwa mpenzi wake Bakari. Baada ya kujiandaa na kuvaa mavazi ya gharama ambayo ,alinunuliwa na mpenzi wake Hamisi.Salma alikuwa amependeza sana.Akaagana na mama yake na kuondoka kuelekea kwa mpenzi wake wa moyoni. Bakari alikuwa chumbani kwake amejipunzisha,kutokana na uchovu wa kazi za kutwa nzima. Salma alipofika nyumba anakoishi Bakari akaenda moja kwa moja na kugonga mlango wa Bakari. Bakari akamkaribisha na wakaenda kitandani kujipunzisha.Salma alikuwa anampenda sana Bakari kupita Bakari anavyompenda Salma. Kwa wakati huo Hamisi alikuwa yupo nyumbani kwake amejipunzisha na mpenzi wake Mwanaidi.Hamisi na Mwanaidi wamekuwa wapenzi kwa zaidi ya miaka kumi.Kuna mengi mafunzo utayapata katika hadithi hii,kuhusiana na vituko na mambo yanayojitokeza kwa wapenzi duniani kote.
<

Sunday, February 10, 2013

RAHA YA MAPENZI NI KUPENDWA(SEHEMU YA 1)

Katika maisha ya upendo,Salma anakutana na kijana mmoja aitwae Hamisi.Ilikuwa ni siku ya jumatatu asubuhi na mapema,wakati jua lilikuwa linachomoza,ndani ya jiji la Mwanza.Watu walikuwa katika pirika pirika za kuelekea kwenye kutafuta riziki.Katika hali isiyo ya kawaida,Hamisi akiwa ni mfanya biashara mkubwa pale mjini Mwanza,anasimamisha gari yake pembeni mwa Barabara,baada ya kumuona msichana mrembo,akiwa anatembea kwa miguu. Hamisi akamsalimia yule msichana,dada habari yako?Yule msichana akamjibu nzuri kaka.Hamisi akamuliza yule msichana,dada naona unatembea kwa miguu,sijui unaitwa nani?msichana akamjibu,naitwa Salma,na wewe unaitwa nani?Yule kaka akamjibu,mimi naitwa Hamisi,unaelekea wapi?Salma akamjibu Hamisi,naelekea mjini.Hamisi akamwambia Salma,hata mimi naelekea mjini.panda twende.Salma akaingia kwenye gari,Hamisi akawaswha gari moto na wakaelekea mjini. Wakiwa njiani,waliweza kuongea maongezi marefu sana,kiasi kwamba walijikuta kana kwamba wanafahamiana kwa muda mrefu sana.Hamisi alitokea kumpenda sana Salma,kutokana na maumbile yake na uzuri wa Salma jinsi ,alivyoumbika. Kwa upande wa salma alionyesha upendo wa wa kumpenda Hamisi,lakini moyoni hapakuwa na upendo zaidi ya kuwa na tamaa na utajiri alionao Hamisi. Hamisi akaegesha gari lake pembeni mwa duka la nguo za kike na manukato.Wakashuka wote kwa pamoja na kuingia kwenye duka la nguo na manukato. Hamisi akamgeukia Salma,napenda ujisikie huru,chagua nguo uipendayo na manukato.pesa ya kulipa ipo usijali.(Sehemu ya pili itaendelea kesho)
http://www.scarlet-clicks.info/banners/banner1.png