Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Monday, April 2, 2012
PENZI LA MASHAKA(SEHEMU YA TATU)
Katika sehemu ya pili,tumeona Saimoni,na Jonas wakiwa wamejipunzisha katika ufukwe wa Bahari,maeneo ya Kunduchi Beach,wakiwa ni watu wenye furaha,walifurahia kuwa pamoja siku ya kwanza kukutana,tokea Saimon,arudi masomoni uingereza,nini (kitaendelea---?)
Ilikuwa ni majira ya saa 4 usiku,Saimon na Jonas,walikodisha gari ndogo,na kurejea nyumbani sinza.Walipofika sinza,Saimon alikuwa amechoka sana,akupoteza muda,akaenda kujipunzisha ,baada ya kuagana na jonas.Saimoni na jonas walikuwa ni majirani wa karibu sana,kuna tofauti ya nyumba tano.Asubuhi na mapema,Saimon aliamka na kujiandaa kwenda kuripoti kwenye kazi,Wakati akiwa masomoni uingereza,Saimoni alikuwa akifanya mpango wa kazi,kwa kupitia kwenye mtandao wa ZOOM.Saimoni aliweza kupata kazi,kwenye kampuni ya Baba yake Anita,ambaye walikwa wote masomoni uingereza na Anita.Saimon alikuwa amekwisha anzisha uhusiano na Anita ,wakati wakiwa masomoni uingereza.Kitu ambacho,Jonas kama atakigunduwa,anaweza,sumu na kujiuwa,kwa jinsi anavyompenda Saimon,inasikitisha kwa mwanaume kama Saimon,kuwa na tabia mbaya ,ya kuwa changanya wanawake wawili,kwa tamaa ya kitu kutoka kwa Anita.Saimon ,alipanda daladala,mpaka pale Bamaga,alipofika pale,akampigia simu Anita,ili aweze kuja mchukuwa.Baada ya kumpigia simu,Anita akawasili pale Bamaga,na kuja kumchukuwa Saimon.(
nini kitaendelea?baada ya muda kidogo,tutaendelea)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment