Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Thursday, April 5, 2012
PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA SITA)
.
Anita na saimon,walianza upendo wao ,wakiwa masomoni uingereza,lakini tokea wamerudi masomoni,mapenzi yao yamekuwa yakishamiri kadri siku zilivyokuwa zikienda mbele,wakiwa mbezi beach,saimon alifurahia mazingira ya mbezi beach,kama yale ,aliyokutana nayo uingereza.Majira ya saa 3 usiku,Anita na Saimon,wakaondoka kurudi nyumbani,Anita aliendesha gari,mpaka Bamaga,na kumshusha mpenzi wake Saimon,Anita akafungua mkoba wake ,na kumpatia Saimon ,kiasi cha shilingi milioni moja,pesa ya matumizi ya Saimon.Baada ya kupokea pesa hizo Saimon,alimshukuru mpenzi wake Anita,wakaagana na Kuachana pale Bamaga.Anita akaelekea nyumbani kwao,wakati Saimon,alikodisha gari ndogo na kumpeleka sinza,nyumbani kwao.Jonas alikuwa nyumbani kwa kina Saimon,akimsubiri ili ,apate kuonana nae,kwa sababu,alikuwa hajaonana nae karibu masaa kumi,kwa hiyo alikuwa hana furaha moyoni mwake.Saimon alipofika pale nyumbani,akashangaa kuonana na Jonas,Saimon akamuliza Jonas,mbona mpaka muda huu,uko hapa?Jonas akamjibu,niko hapa kwa sababu,sijakuona mpenzi wangu,tokea asubuhi?(nini kitatokea?tutaendelea baada ya muda mfupi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment