Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Saturday, April 7, 2012
PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA TATU)
Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon na Jonas,wakiwa pamoja na kubadilishana mawazo pale chumbani.Baada ya maongezi ya muda mrefu,usingizi ukawachukuwa.(sasa endelea.....)
Ilikuwa majira ya saa kumi na moja asubuhi,Saimon aliamka na mapema,akaenda bafuni kujimwagia maji,na kujiandaa kwa ajili ya kwenda mjini,na kisha kwenda kuonana na Anita.Saimon akajitayarisha na kuagana na Jonas.Saimon akaondoka na kuelekea mjini kuonana na peter.Alipofika mjini akakutana na peter.wakazungumza kwa muda mrefu,kisha peter akamwambia Saimon,naomba ufike nyumbani kesho,tupate chakula cha mchana.Saimon akamjibu,sawa nitakuja kesho,mapema ili tupate muda mwingi wa kuongea.Saimon akaondoka na kuelekea Bamaga.Alipofika pale,akampigia simu Anita.Baada ya muda mfupi ,Anita akawasili na kumkuta Saimon,akiwa anamsubiri pale nje.Wakatafuta sehemu ya pembeni na kukaa chini,wakajipunzisha.Anita akamwambia Saimon,mipango yetu ya kufungua kiwanda imekamilika,pesa nimeipata tayari.Saimon akatabasamu kusikia habari kama hiyo.Saimon akamuliza Anita,tutaanza maandalizi lini?Anita akamjibu,itabidi kwanza uwende kenya,kuangalia wapi tutapata vifaa vya kuwekea juice.Saimon akamjibu Anita,mimi niko tayari hata kesho kwenda kenya.Anita akamwambia Saimon,kama uko tayari kesho kwenda,itabidi nikukatie tiketi ya ndege kesho asubuhi uwende.Anita na Saimon, wakaelekea benki na kuchukuwa pesa ya kutosha.Baada ya hapo Anita ,akatoa kiasi cha shilingi milioni moja na kumpatia Saimon,kwa ajili ya kuwachia nyumbani kwao.(nini kitatokea?tutaendelea baada ya muda)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment