Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Saturday, April 7, 2012
PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA MBILI)
Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon na peter,wakikutana na kupanga kwenda mjini asubuhi na mapema,Saimon alikuwa amechoka sana,akaenda kujipunzisha kitandani,majira ya jioni.(sasa endelea...)
Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni,Jonas akaondoka na kuelekea nyumbani kwa Saimon.Alipofika nyumbani kwa kina Saimon,akamkuta Saimon amejipunzisha kitandani.Jonas akaenda mpaka kitandani na kujitupa kwenye kitanda.Jonas akajipunzisha pale kitandani na usingizi ukamchukuwa pale pale kitandani.Majira ya saa mbili usiku,Saimon akashtuka kutoka usingizini,akashangaa kumkuta jonas,akiwa amelala pale kitandani.Kwa wakati huo,Jonas alikuwa na usingizi mzito,hakuweza kushtuka.Saimon akaenda bafuni kujimwagia maji,na kurudi chumbani.Baada ya muda kupita Jonas ,akashtuka kutoka usingizini,na kumkuta Saimon,akiwa amekaa kwenye sofa ,pale chumbani.Jonas akaondoka pale kitandani na kwenda kumfuata Saimon kwenye sofa.Jonas na Saimon,wakakumbatiana na kisha Saimon akamwambia Jonas,nimekumic sana mpenzi wangu.Jonas akamjibu,hata mimi mpenzi wangu nimekumic sana.Saimon akaenda jikoni,kuangalia kama kuna chakula,akakuta mama yake,amempikia wali na nyama.Saimoni akapakuwa chakula na kwenda mpaka chumbani,akachukuwa kijiko kimoja,akampa Jonas na wakaanza kula chakula kwenye sahani moja.Baada ya kumaliza kula chakula,wakaenda kulala pamoja chumbani.Saimon akamuliza Jonas,unapenda maisha yetu yawe,maisha yetu,tuishi maisha ya namna gani?Jonas akamuliza Saimon,sijaelewa swali lako,Saimon akarudia swali lake kwa Jonas,akamuliza Jonas,napenda kujuwa mimi na wewe,tutaishi maisha ya namna gani?Jonas akamjibu Saimon,tutaishi maisha ya shida na raha,usijali kwa kila kitu.Saimon na Jonas waliendelea na maongezi yao,mpaka usingizi ukawachukuwa.(nini kitatokea...)angalia sehemu inayofuata,baada ya muda mfupi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment