Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Saturday, April 7, 2012
PENZI LA MASHAKA ( SEHEMU YA KUMI)
Katika sehemu iliyopita tumeona,Anita na Saimon,wakiwa mbezi beach,na kukubaliana kuhusu shauri lao,la kufunga ndoa,baada ya Saimon,kumuelezea yanamtatiza au pingamizi lake,linamfanya awe mzito katika kukamilisha swala zima la ndoa.(sasa endelea....)
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu,Saimon na Anita,wakakubaliana na swala la ndoa.Saimon na Anita wakakubaliana kununua nyumba ,maeneo ya masaki.Saimon akamshauri Anita ,wafungue kiwanda cha kutengeneza juice.Anita akakubaliana na ,ushauri wa Saimon ,wakafanya uchunguzi wa jinsi ya kufanya biashara ya kusambaza juice,kutoka kiwandani kwao.Anita akamwambia Saimon,vipi kuhusu vifaa vya kuwekea juice na wapi tutaweza kupata matunda kwa wingi?Saimon akamjibu,tunaweza kuagiza vifaa ,kutoka nchi jirani ya kenya.ila matunda ,tunaweza kupata maeneo ya Tanga,Morogoro na Arusha.Tutakuwa na malori yetu,ambayo yatakwenda mikoani,na kununua matunda kwa wananchi kila siku.Baada ya maongezi marefu,Anita na Saimon,wakaagana na kuelekea nyumbani.Saimon akaelekea Sinza ,baada ya kushuka pale Bamaga.Saimon alipofika nyumbani,akakutana na rafiki yake peter,amekuja kumtafuta ili,waende mjini kutembea.Peter akasalimiana na Saimon,Baada ya kusalimiana,Peter akamwambia Saimon,nimekuja kukuona,nikaambiwa na mama yako,umetoka ila hautachelewa kurudi.(nini kitatokea?baada ya muda mfupi,tutaendelea)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment