Hadithi za kwetu,ni mchanganyiko wa hadithi za mapenzi na matukio mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania,Mtakuwa mkipata hadithi kila siku katka Blog hii ya Hadithi za kwetu.Yako mambo mengi ya kujifunza katika Blog hii,ambayo jamii,itaweza kujifunza kutokana na matukio mengi,yanayotokea kila siku kwenye jamii.Nina imani,tutakuwa pamoja na kujenga ushirikiano,katika kufanikisha kila kitu,kinaenda sawa,karibuni wote kwenye Blog ya hadithi za kwetu.
Translate
Saturday, April 7, 2012
PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA TISA)
Katika sehemu iliyopita tumeona saimon na jonas ,wakiwa wamelala pamoja,katika usiku uliokuwa wa mawazo makubwa kwa Saimon,ilipofika asubuhi,alijiandaa kwenda kazini,lakini kabla ya kuondoka,akampatia jonas,shilingi laki moja.(sasa endelea...)
Saimon akaondoka kuelekea Bamaga,alipofika akampigia simu,Anita,na kumjulisha ya kwamba amekwishafika pale Bamaga.Anita akawasha gari moto na kuenda kumfuata Saimon,Anita akaendesha gari taratibu mpaka pale,Bamaga.Baada ya kusalimiana na Saimon ,wakaondoka pamoja na kuelekea mbezi beach.walipofika mbezi beach,kama kawaida yao,wakaagiza nyama choma,na vinywaji.Baada ya muda mfupi,Anita akamwambia Saimon,mimi nakupenda sana,ningependa tufunge ndoa mwaka huu,utakuwa tayari kwa hilo?Saimon akamjibu,mimi napenda uwe mke wangu,lakini tatizo,ni kwamba,mimi ni maskini,isitoshe,katika familia yangu,wote wananitegemea mimi,itakuwa ngumu ,kuwasaidia wakati huu,nikiwa sina kazi yeyote.Anita akamuliza,kwani tatizo lao,ni nini?au ungependa nikufanyie nini,ili tuweze kufunga ndoa?Saimon akamwambia Anita.mimi napenda niwajengee nyumba,halafu niwafungulie mradi wa vifaranga vya kuku.Anita akamjibu Saimon,nitakutimizia yote hayo,kaa chini unipe mahesabu kamili.Saimon akamjibu,Anita usiwe na wasiwasi ,nitakujibu baada ya siku 2.(nini kitaendelea....soma sehemu inayofuata baada ya muda mfupi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment