Translate

Saturday, April 21, 2012

PENZI LA MASHAKA(SEHEMU YA KUMI NA TANO)

Katika sehemu iliyopita tumejaribu kuwaeleza mwenendo mzima wa taswira ya hadithi hii,na tuliangalia pia ,Saimon na Anita ,walipokutana na kisha baada ya maongezi,wakaagana,kila mmoja kurejea nyumbani kwake.(sasa endelea...) Saimon na Jonas ,walikuwa kwenye maongezi chumbani,Jonas alikuwa ni msichana mwenye huruma na mpole.Jonas ni msichana mvumilivu na mwenye maadili mema kwa kila mtu.Saimon alikuwa na pesa nyingi mfukoni,akachukuwa pesa zake na kumpatia Jonas.Baada ya muda kidogo Anita akampigia simu Saimon,kwa wakati huo,Saimon alikuwa amekumbatiana na Jonas kitandani.Jonas akapokea simu ya Saimon,Anita kama kawaida yake ,akamsalimia Saimon,Habari yako Saimon?Jonas akamuliza nani wewe?Anita akamjibu ,kwani wewe ni nani?Jonas akamwambia Anita,unajuwa wewe msichana mkorofi sana,umepiga kwenye simu ya bwana wangu,halafu nakuliza nani wewe,unashindwa kunijibu,badala yake ,unaniuliza mimi nani?Kwa wakati huo,Saimon alikuwa kimya akisikiliza mazungumzo kati ya wapenzi wake wawili.Saimon hakuweza kuongea lolote mpaka ,maongezi yalipokwisha.Jonas akaweka simu ya Saimon mezani ,na akarudi kitandani alipokuwa Saimon.baada ya muda sio mrefu,usingizi ukawachukuwa na wakjikuta wamelala usingizi mzito. Asubuhi na mapema,Saimon akajiandaa kuelekea bamaga,ili aweze kuwasiliana na Anita,Saimon akatoka nyumbani kwake,wakati akiwa kituoni kuelekea bamaga,Anita akampigia simu Saimon,Baada ya kusalimiana ,Anita akamuliza Saimon,mbona unawapa simu yako,hao wanawake zako?Saimon akamjibu Anita ,samahani sana,jana kulikuwa na dharura kidogo,(itaendelea....)

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA NNE)

Katika sehemu iliyopita tumeona saimon na jonas wakiwa pamoja usiku mzima,kisha saimon alikwenda mjini asubuhi na mapema,baada ya kufika mjini akakutana na Peter,wakapata muda wa kuongea na kuagana,kisha Saimon akaelekea Bamaga,alipofika akampigia simu Anita,ili waweze kukutana na kupanga mikakati ya kazi .sasa endelea..) Kama tunavyoelewa binadam huwa anabadilika kadri mazingira yanavyobadil
ika,kama ulikuwa makini mwanzo wa hadithi hii,utaona jonas na Saimon ,walikuwa wapenzi tokea mwanzo wa hadithi,kabla ya Saimon hajaenda uk ,kusoma.Lakini Saimon yule wa mwanzo ,siye Saimon wa leo,Amekuwa anabadilika kadri siku zinavyoenda mbele,Ukiangalia kwa undani kabisa,utaona Jonas ni msichana mvumilivu na mwenye upendo wa dhati kwa Saimon,hivyo inamfanya Saimon kuwa mzito katika maamuzi yake,ya kumchagua mpenzi mmoja kati ya Jonas na Anita.Lakini ukifuatilia kwa makini utaona Saimon yupo karibu na Anita kwa sababu ya tamaa ya mali,na si tamaa ya mapenzi.Hii ndio hali halisi ya maisha ya sasa,na ndio imenivuta kwa undani zaidi kuandika hadithi hii,Lengu langu haswa ni kuwakumbusha wote walio katika jamii,kuwa na msimamo na wapenzi wao,hata kama hawana kitu,kwa kufanya hivyo,mtaweza kuwa na mapenzi ya dhati na yenye furaha.Saimon akampigia simu Anita ,wakaagana kukutana bamaga.Waliweza kupanga mambo yao ya kazi,baada ya hapo,Anita akampatia Saimon pesa ya matumizi.Wakaagana na kila mmoja akarejea nyumbani kwake.Saimon alipofika sinza akakutana na Jonas,wakasalimiana kisha wakaenda chumbani kujipunzisha,walipokuwa chumbani,Jonas akamuliza Saimon,vipi leo,mbona umechelewa?Saimon akamjibu,nilikuwa na kazi nyingi,ndio maana nimechelewa.(itaendelea....)

Saturday, April 7, 2012

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA TATU)

Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon na Jonas,wakiwa pamoja na kubadilishana mawazo pale chumbani.Baada ya maongezi ya muda mrefu,usingizi ukawachukuwa.(sasa endelea.....) Ilikuwa majira ya saa kumi na moja asubuhi,Saimon aliamka na mapema,akaenda bafuni kujimwagia maji,na kujiandaa kwa ajili ya kwenda mjini,na kisha kwenda kuonana na Anita.Saimon akajitayarisha na kuagana na Jonas.Saimon akaondoka na kuelekea mjini kuonana na peter.Alipofika mjini akakutana na peter.wakazungumza kwa muda mrefu,kisha peter akamwambia Saimon,naomba ufike nyumbani kesho,tupate chakula cha mchana.Saimon akamjibu,sawa nitakuja kesho,mapema ili tupate muda mwingi wa kuongea.Saimon akaondoka na kuelekea Bamaga.Alipofika pale,akampigia simu Anita.Baada ya muda mfupi ,Anita akawasili na kumkuta Saimon,akiwa anamsubiri pale nje.Wakatafuta sehemu ya pembeni na kukaa chini,wakajipunzisha.Anita akamwambia Saimon,mipango yetu ya kufungua kiwanda imekamilika,pesa nimeipata tayari.Saimon akatabasamu kusikia habari kama hiyo.Saimon akamuliza Anita,tutaanza maandalizi lini?Anita akamjibu,itabidi kwanza uwende kenya,kuangalia wapi tutapata vifaa vya kuwekea juice.Saimon akamjibu Anita,mimi niko tayari hata kesho kwenda kenya.Anita akamwambia Saimon,kama uko tayari kesho kwenda,itabidi nikukatie tiketi ya ndege kesho asubuhi uwende.Anita na Saimon, wakaelekea benki na kuchukuwa pesa ya kutosha.Baada ya hapo Anita ,akatoa kiasi cha shilingi milioni moja na kumpatia Saimon,kwa ajili ya kuwachia nyumbani kwao.(nini kitatokea?tutaendelea baada ya muda)

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA MBILI)

Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon na peter,wakikutana na kupanga kwenda mjini asubuhi na mapema,Saimon alikuwa amechoka sana,akaenda kujipunzisha kitandani,majira ya jioni.(sasa endelea...) Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni,Jonas akaondoka na kuelekea nyumbani kwa Saimon.Alipofika nyumbani kwa kina Saimon,akamkuta Saimon amejipunzisha kitandani.Jonas akaenda mpaka kitandani na kujitupa kwenye kitanda.Jonas akajipunzisha pale kitandani na usingizi ukamchukuwa pale pale kitandani.Majira ya saa mbili usiku,Saimon akashtuka kutoka usingizini,akashangaa kumkuta jonas,akiwa amelala pale kitandani.Kwa wakati huo,Jonas alikuwa na usingizi mzito,hakuweza kushtuka.Saimon akaenda bafuni kujimwagia maji,na kurudi chumbani.Baada ya muda kupita Jonas ,akashtuka kutoka usingizini,na kumkuta Saimon,akiwa amekaa kwenye sofa ,pale chumbani.Jonas akaondoka pale kitandani na kwenda kumfuata Saimon kwenye sofa.Jonas na Saimon,wakakumbatiana na kisha Saimon akamwambia Jonas,nimekumic sana mpenzi wangu.Jonas akamjibu,hata mimi mpenzi wangu nimekumic sana.Saimon akaenda jikoni,kuangalia kama kuna chakula,akakuta mama yake,amempikia wali na nyama.Saimoni akapakuwa chakula na kwenda mpaka chumbani,akachukuwa kijiko kimoja,akampa Jonas na wakaanza kula chakula kwenye sahani moja.Baada ya kumaliza kula chakula,wakaenda kulala pamoja chumbani.Saimon akamuliza Jonas,unapenda maisha yetu yawe,maisha yetu,tuishi maisha ya namna gani?Jonas akamuliza Saimon,sijaelewa swali lako,Saimon akarudia swali lake kwa Jonas,akamuliza Jonas,napenda kujuwa mimi na wewe,tutaishi maisha ya namna gani?Jonas akamjibu Saimon,tutaishi maisha ya shida na raha,usijali kwa kila kitu.Saimon na Jonas waliendelea na maongezi yao,mpaka usingizi ukawachukuwa.(nini kitatokea...)angalia sehemu inayofuata,baada ya muda mfupi)

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA KUMI NA MOJA)

Katika sehemu iliyopita tumeona ,Anita na Saimon,wakipanga mikakati ya kufungua kiwanda cha juice,na jinsi ya kuendesha biashara yao,Baada ya kuweka mikakati yao.Wakaagana na kurudi nyumbani.Alipofika nyumbani Sinza akakutana na rafiki yake peter.Baada ya kusalimiana,Peter akamwambia Saimon,nimekuja muda kidogo,ila mama yako,aliniambia umetoka na hautachelewa kurudi.(sasa endelea....) Saimon alikuwa amechoka sana,Akamwambia peter,najisikia nimechoka sana,sitaweza kutoka muda huu,labda tungefanya kesho asubuhi.Peter akamjibu saimon,usiwe na wasiwasi punzika,tutaeta kesho.Peter akamuaga Saimon na kuelekea nyumbani kwake Kariakoo.Peter alikuwa ni mtu wake wa karibu Saimon,tokea kipndi chao,walichokuwa wakisoma shule ya msingi.Peter alikuwa hodari sana shuleni,katika micezo ya maigizo,kwa hivi sasa,amekuwa akijishughulisha na kutunga nyimbo za bongo fleva.Peter ana watoto wawili wakike.mmoja anaitwa Anna,mwenye miaka 19,mwengine ni Esther mwenye miaka 21.Saimon alikwenda bafuni,kwa ajili ya kujimwagia maji,baada ya kujimwagia maji,akaenda kujipunzisha chumbani kwake.Ilikuwa ni majira ya saa kumi jioni,wakati Saimon alipokwenda kujipunzisha kitandani.Jonas alikuwa ni msichana aliyevutwa sana na Saimon,kwa wakati huo alikuwa yupo nyumbani kwao,ila mawazo yote,yalikuwa ni kwa Saimon.Jonas akajitayarisha kwa kuoga,na kujiandaa kwenda kumwona Saimon nyumbani kwao.(nini kitatokea?tutaendelea...)

PENZI LA MASHAKA ( SEHEMU YA KUMI)

Katika sehemu iliyopita tumeona,Anita na Saimon,wakiwa mbezi beach,na kukubaliana kuhusu shauri lao,la kufunga ndoa,baada ya Saimon,kumuelezea yanamtatiza au pingamizi lake,linamfanya awe mzito katika kukamilisha swala zima la ndoa.(sasa endelea....) Baada ya mazungumzo ya muda mrefu,Saimon na Anita,wakakubaliana na swala la ndoa.Saimon na Anita wakakubaliana kununua nyumba ,maeneo ya masaki.Saimon akamshauri Anita ,wafungue kiwanda cha kutengeneza juice.Anita akakubaliana na ,ushauri wa Saimon ,wakafanya uchunguzi wa jinsi ya kufanya biashara ya kusambaza juice,kutoka kiwandani kwao.Anita akamwambia Saimon,vipi kuhusu vifaa vya kuwekea juice na wapi tutaweza kupata matunda kwa wingi?Saimon akamjibu,tunaweza kuagiza vifaa ,kutoka nchi jirani ya kenya.ila matunda ,tunaweza kupata maeneo ya Tanga,Morogoro na Arusha.Tutakuwa na malori yetu,ambayo yatakwenda mikoani,na kununua matunda kwa wananchi kila siku.Baada ya maongezi marefu,Anita na Saimon,wakaagana na kuelekea nyumbani.Saimon akaelekea Sinza ,baada ya kushuka pale Bamaga.Saimon alipofika nyumbani,akakutana na rafiki yake peter,amekuja kumtafuta ili,waende mjini kutembea.Peter akasalimiana na Saimon,Baada ya kusalimiana,Peter akamwambia Saimon,nimekuja kukuona,nikaambiwa na mama yako,umetoka ila hautachelewa kurudi.(nini kitatokea?baada ya muda mfupi,tutaendelea)

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA TISA)

Katika sehemu iliyopita tumeona saimon na jonas ,wakiwa wamelala pamoja,katika usiku uliokuwa wa mawazo makubwa kwa Saimon,ilipofika asubuhi,alijiandaa kwenda kazini,lakini kabla ya kuondoka,akampatia jonas,shilingi laki moja.(sasa endelea...) Saimon akaondoka kuelekea Bamaga,alipofika akampigia simu,Anita,na kumjulisha ya kwamba amekwishafika pale Bamaga.Anita akawasha gari moto na kuenda kumfuata Saimon,Anita akaendesha gari taratibu mpaka pale,Bamaga.Baada ya kusalimiana na Saimon ,wakaondoka pamoja na kuelekea mbezi beach.walipofika mbezi beach,kama kawaida yao,wakaagiza nyama choma,na vinywaji.Baada ya muda mfupi,Anita akamwambia Saimon,mimi nakupenda sana,ningependa tufunge ndoa mwaka huu,utakuwa tayari kwa hilo?Saimon akamjibu,mimi napenda uwe mke wangu,lakini tatizo,ni kwamba,mimi ni maskini,isitoshe,katika familia yangu,wote wananitegemea mimi,itakuwa ngumu ,kuwasaidia wakati huu,nikiwa sina kazi yeyote.Anita akamuliza,kwani tatizo lao,ni nini?au ungependa nikufanyie nini,ili tuweze kufunga ndoa?Saimon akamwambia Anita.mimi napenda niwajengee nyumba,halafu niwafungulie mradi wa vifaranga vya kuku.Anita akamjibu Saimon,nitakutimizia yote hayo,kaa chini unipe mahesabu kamili.Saimon akamjibu,Anita usiwe na wasiwasi ,nitakujibu baada ya siku 2.(nini kitaendelea....soma sehemu inayofuata baada ya muda mfupi)

Thursday, April 5, 2012

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA NANE)

Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon akirudi nyumbani na kukutana na Jonas,akimsubiri,Saimon na Jonas ,baada ya kusalimiana na kuelekea chumbani ,kwa ajili ya kulala.Majira ya saa 5 usiku,Anita akampigia simu,Saimon,Lakini ilikuwa ni vigumu kw saimon kupokea simu.Saimon akachukuwa taulo,na kuelekea bafuni.hapo ndipo Jonas,akamfuata Saimon nyuma,bila kuelewa.Saimon na Anita,wakati wakiwa kwenye mazungumzo,Jonas alikuwa akiwasikiliza.(Nini kitatokea?sasa endelea...)Jonas
akaendelea kusikiliza mazungumzo,mpaka walipomaliza maongezi yao,Jonas akakimbia chumbani,alipofika chumbani,akajitupa kitandani na kuanza kukoroma,kama mtu ,aliyekuwa amelala muda mrefu uliyopita.Saimon alipomaliza maongezi bafuni,akajimwagia maji,na kurudi chumbani.Alipofika chumbani,akamkuta Jonas akiwa hoi,amelala.Saimon akajisemea moyoni,nina kazi ngumu ya kuchagua mpenzi bora kwangu.Saimon akajitupa kitandani,na kuanza kulala.Ilipofika asubuhi,majira ya saa moja asubuhi,Saimon aliamka,na kuanza kujiandaa kwa ajiki ya kwenda kazini.Saimon akamwambia Jonas,usiwe na wasiwasi mpenzi,naelekea kazini,lakini ngoja nikupe pesa ya matumizi.Saimon akatoa shilingi laki moja,na kumpatia Jonas.(nini kitatokea?tutaendele,baada ya mfupi.

PENZI LA MASHAKA ( SEHEMU YA SABA)

Baada ya kuagana saimon na Anita,Saimon anfika nyumbani na kukutana na mpenzi wake mwengine Jonas,akiwa nyumbani anamsubiri.(sasa endelea...) Jonas alikuwa mwenye furaha baada ya kumwona Saimon,akiwa amerejea nyumbani salama.Lakini Saimon,alikuwa mwenye kukerwa na uamuzi wa Jonas ,kukaa mpaka majira ya saa 5 usiku,akiwa anamsubiri.Lakini alijikaza kiume,kiasi kwamba Jonas ,akuelewa kitu gani ,anakifiki
ria Saimon ,kwa muda ule.Saimon akamwambia Jonas,twende chumban tukalale ,muda mwingi umeenda.Jonas akamuliza Saimon,itakuwaje mama yako,akiniona nimelala na wewe ndani ya chumba chako?Saimon akamjibu,usiwe na wasiwasi,niko tayari kwa lolote.Jonas akamwambia Saimon ,sawa twende tukalale.Wakaingia chumbani,kwa ajili ya kujipunzisha.Baada ya muda mfupi wakiwa wamelala kitandani,Ilikuwa mjira ya saa 5,Anita akampigia simu Saimon,simu ilikuwa inaita,Saimon akachukuwa taulo,na kuelekea bafuni,ili aweze kuongea vizuri na Anita.Jonas alipoona Saimon,anaelekea bafuni,akaenda kumfuata nyuma,kimya kimya,bila Saimon kujua.Jonas akajibanza pembeni mwa ukuta wa bafuni,lakini ilikuwa ni sehemu aliyokuwa akisikia maongezi ya simu vizuri.(nini kitatokea?tutaendelea baada ya muda kidogo)

PENZI LA MASHAKA (SEHEMU YA SITA)

. Anita na saimon,walianza upendo wao ,wakiwa masomoni uingereza,lakini tokea wamerudi masomoni,mapenzi yao yamekuwa yakishamiri kadri siku zilivyokuwa zikienda mbele,wakiwa mbezi beach,saimon alifurahia mazingira ya mbezi beach,kama yale ,aliyokutana nayo uingereza.Majira ya saa 3 usiku,Anita na Saimon,wakaondoka kurudi nyumbani,Anita aliendesha gari,mpaka Bamaga,na kumshusha mpenzi wake Saimon,Anita akafungua mkoba wake ,na kumpatia Saimon ,kiasi cha shilingi milioni moja,pesa ya matumizi ya Saimon.Baada ya kupokea pesa hizo Saimon,alimshukuru mpenzi wake Anita,wakaagana na Kuachana pale Bamaga.Anita akaelekea nyumbani kwao,wakati Saimon,alikodisha gari ndogo na kumpeleka sinza,nyumbani kwao.Jonas alikuwa nyumbani kwa kina Saimon,akimsubiri ili ,apate kuonana nae,kwa sababu,alikuwa hajaonana nae karibu masaa kumi,kwa hiyo alikuwa hana furaha moyoni mwake.Saimon alipofika pale nyumbani,akashangaa kuonana na Jonas,Saimon akamuliza Jonas,mbona mpaka muda huu,uko hapa?Jonas akamjibu,niko hapa kwa sababu,sijakuona mpenzi wangu,tokea asubuhi?(nini kitatokea?tutaendelea baada ya muda mfupi)

Monday, April 2, 2012

PENZI LA MASHAKA(SEHEMU YA TANO)

Katika sehemu iliyopita,tumeona Anita na Saimon,wakiwa Bamaga,baada ya kukutana,na kuongea kwa kifupi(,sasa endelea...) Anita akamwambia Saimon,napenda tuwe wote siku ya leo,kwenye maeneo ya mbezi beach,Saimon akamjibu mmhhh,,,sasa vipi kuhusu kazi itakuwaje?Anita akamjibu,wasiwasi wako wewe nini?Saimon akamjibu Anita,sina wasiwasi,ila nategemea hiyo kazi,ndio itakuwa mkombozi wangu.Anita akacheka sana,kisha akamwambia Saimon,mimi ndio meneja wako,nitakupa utakachokitaka.Saimon akamwambia Anita,unajuwa mimi nina familia,na isitoshe nyumbani sisi ni masikini sana,siwezi nikakuomba kila kitu,inaweza kuwa ni tatizo kwangu.Anita akamwambia Saimon,twende mbezi beach,nitakupatia pesa,ukatatuwe matatizo ya nyumbani kwenu.Saimon kwa shingo upande,akakubali,akamwambia Anita,sawa mimi naona bora twende.
SAIMON NA MPENZI WAKE ANITA
Saimon na Anita,wakaondoka pamoja na kuelekea mbezi beach.wakiwa mbezi beach,waliagiza vinywaji na nyama ya kuchoma.wakiwa wanakula na kunywa,Saimon alikuwa anatabasam,Anita akamuuliza saimon,mbona umefurahi sana mpenzi wangu?Nimefurahi sana,kwa sababu nakupenda sana,ila khofu yangu mimi,sikutegemea kama ungenikubalia penzi lako. Anita akamjibu Saimon,mimi nakupenda sana,na sikutegemea kama ungelikubali penzi langu,lakini umenikubalia,usiwe na wasiwasi,nitakusaidia kwa matatizo yako,na nina imani,utafurahia penzi langu,nakupenda kuliko hata asali.

PENZI LA MASHAKA(SEHEMU YA NNE)

Katika sehemu iliyopita tumeona Saimon,wakiwa wamejipunzisha kunduchi.Majira ya saa 4 usiku,wakaondoka na kurudi nyumbani Sinza.Baada ya kufika nyumbani,wakaagana na Jonas,akarudi nyumbani kwake,Saimon ,aliamka mapema na kuelekea kwenye kazi,katika kampuni ya Baba yake Anita.Saimon alipanda daladala mpaka Bamaga,kisha akampigia simu Anita.(Sasa endelea....) Anita akawasha gari moto na kuelekea Bamaga,Alipofika pale ,akamkuta Saimon amekaa nje,ana msubiri .Anita akasogeza gari lake mpaka pale ,walipokuwa amekaa Saimon,Akashuka kwenye gari,na kumkumbatia Saimon.
Anita na Saimon,wakakaa chini na kuanza kuongea kuhusu mipango ya kazi.Anita akamwambia Saimon,kuhusu mipango ya kazi,usiwe na wasiwasi,nimemwambia Baba,khusu wewe,na amekubali ,ukafanye kazi kwenye kiwanda chake cha kutengeneza software za catoon,ukiwa kama meneja msaidizi.Mimi ndio meneja.Saimon akafurahi sana kusikia hivyo,Anita akamwambia Saimon,unajuwa mimi,nakupenda sana,ndio maana ,nimefanya mipango yote,nategemea wewe ndio uwe wangu mpenzi,Kabla ya yote ,nakupa zawadi nzuri ya uwa,kuashiria kwamba,sina mwengine zaidi yako.
Simon alifurahi sana,kwa zawadi ya uwa la rosi,kuashiria alama ya upendo,kutoka kwa Anita,(nini kitaendelea?Tukutane tena baada ya muda mfupi.

PENZI LA MASHAKA(SEHEMU YA TATU)

Katika sehemu ya pili,tumeona Saimoni,na Jonas wakiwa wamejipunzisha katika ufukwe wa Bahari,maeneo ya Kunduchi Beach,wakiwa ni watu wenye furaha,walifurahia kuwa pamoja siku ya kwanza kukutana,tokea Saimon,arudi masomoni uingereza,nini (kitaendelea---?) Ilikuwa ni majira ya saa 4 usiku,Saimon na Jonas,walikodisha gari ndogo,na kurejea nyumbani sinza.Walipofika sinza,Saimon alikuwa amechoka sana,akupoteza muda,akaenda kujipunzisha ,baada ya kuagana na jonas.Saimoni na jonas walikuwa ni majirani wa karibu sana,kuna tofauti ya nyumba tano.Asubuhi na mapema,Saimon aliamka na kujiandaa kwenda kuripoti kwenye kazi,Wakati akiwa masomoni uingereza,Saimoni alikuwa akifanya mpango wa kazi,kwa kupitia kwenye mtandao wa ZOOM.Saimoni aliweza kupata kazi,kwenye kampuni ya Baba yake Anita,ambaye walikwa wote masomoni uingereza na Anita.Saimon alikuwa amekwisha anzisha uhusiano na Anita ,wakati wakiwa masomoni uingereza.Kitu ambacho,Jonas kama atakigunduwa,anaweza,sumu na kujiuwa,kwa jinsi anavyompenda Saimon,inasikitisha kwa mwanaume kama Saimon,kuwa na tabia mbaya ,ya kuwa changanya wanawake wawili,kwa tamaa ya kitu kutoka kwa Anita.Saimon ,alipanda daladala,mpaka pale Bamaga,alipofika pale,akampigia simu Anita,ili aweze kuja mchukuwa.Baada ya kumpigia simu,Anita akawasili pale Bamaga,na kuja kumchukuwa Saimon.(
nini kitaendelea?baada ya muda kidogo,tutaendelea)

Sunday, April 1, 2012

PENZI LA MASHAKA ( SEHEMU YA PILI)

Katika sehemu iliyopita ,tumeona ,Saimon akirudi masomoni uingereza na kupokewa na mama yake pale mwalimu nyerere.Baada ya kupokewa,wakaelekea pale nyumbani sinza.(sasa endelea....) Saimon na jonas,walikuwa marafiki wakubwa,kabla ya saimon,kwenda masomoni uingereza.Saimon alikuwa na shauku ya kuanzisha uhusiano tena na jonas,baada ya kutengana kwa muda wa miaka minne,wakati alipokuwa masomoni uingereza.Saimoni akamuuliza jonas,tunaelekea wapi jioni hii ?Jonas akamjibu saimoni,popote utakapopenda tutakwenda,Saimoni akamwambia jonas,mimi naona bora ,tungekwenda kupunzika maeneo ya kunduchi beach.Jonas akamjibu saimoni,sawa saimoni,akatoka nje na kukodisha gari,Jonas akatoka njena wakaelekea maeneo ya kunduchi beach Waliwasili pale kunduchi,majira ya saa 12 jioni,na kupata maeneo ya kujipunzisha,kandokando ya ufukwe wa bahari,mbele kidogo ya hoteli ya kunduchi beachi.Waliweza kuongea kwa muda mrefu na kukumbushana katika enzi zile ,waliokuwa wakikutana ,kabla ya saimon,hajaenda kusoma uingereza. Maisha ya wawili hawa,walikuwa na upendo wa dhati,kutoka moyoni,Walipendana kikweli kweli,tokea moyoni.Saimoni akamwambia jonas,nategemea kuanza kazi,hivi karibuni katika kampuni moja hapa mjini,ila nilikuwa na mipango ,ya kufunga ndoa na wewe,ulikuwa unasemaje?Jonas akamjibu,Saimon,nitafurahi,kama itakuwa hivyo.Saimon alikuwa anampenda sana jonas,lakini sio kwa muda huu,lengo la kumdanganya jonas,ni kutaka kumrubuni kimapenzi jonas.Lakini katika mawazo yake Saimoni,anafikiria jengine.nini kitatokea?kuwa nami tena kesho,katika sehemu ya tatu.

PENZI LA MASHAKA ( SEHEMU YA KWANZA)

Katika penzi la mashaka ,tunaangalia pale,Saimon alipokuwa anatoka masomoni uingereza,akiwa amechukuwa shahada ya uchumi,katika chuo kikuu cha OXFORD ya UK.Akiwa katika Airport ya Mwalimu nyerere,Saimon,alipokelewa na rafiki yake,Jonas,pamoja na mama yake Frida.Wote walipakia kwenye gari na kuelekea Sinza ,nyumbani kwa mama yake Saimon.Walipokuwa nyumbani Sinza,Saimon alitembelewa na marafiki zake

mbalimbali,wakiwemo marafiki zake,waliosoma wote pale,shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa.Siku hiyo ilikuwa,ni siku ya furaha kwa Saimoni,pamoja na marafiki zake,Baada ya chakula cha mchana,Saimoni alijipunzisha chumbani,kutokana na uchovu wa safari.Ilipofika majira ya saa 11 jioni,Saimon aliamka na kuenda kujimwagia maji,Baada ya hapo,akapata muda wa kula chakula cha jioni.Baada ya chakula,wakaa na ndugu zake sebuleni,na kuanza kuongea,habari za safari,pamoja na masomo,pale uingereza,Saimon alikuwa ni mtu mwenye furaha sana ,katika siku ile,kwa sababu ilikuwa ,ni siku ya kwanza kutua akitokea uingereza,alikuwa amekaa huko kwa muda wa miaka minne,alikuwa ni mtu mwenye furaha sana,kukutana na marafiki zake na familia kwa ujumla. ( itaendelea.....)